IDARA YA KISWAHILI
IDARA YA KISWAHILI
Karibu sana kwa Idara ya Kiswahili hapa Chuo cha Ufundi cha Mtakatifu Yosefu. Katika idara hii kuna walimu wawili ambao ni Bwana. Anziya Benjamin na BI. Mukhone k.Christabel.
Idara ya Kiswahili ni Idara ndogo na mpya sana hapa chuoni .Baada ya Wizara ya vyuo vya Ufundi miaka miwili iliyopita kutangaza kuwa Kiswahili ni somo la lazima kwa wanafunzi wote wa mwaka wa pili katika vyuo vyote vya ufundi hapa nchini Uganda, St.Joseph kama vyuo vingine hapa nchini walianzisha somo hili.
Wanafunzi wote wa mwaka wa pili hapa Chuoni wanasoma somo hili la Kiswahili.
Tunamshukuru mwalimu wetu mkuu mpendwa Bwana.Iga David kwa kufuata agizo hili la Wizara na kuanzisha somo la Kiswahili hapa Chuoni. Asante sana bwana.
Sisi kama walimu wa lugha ya Kiswahili, tunapenda sana kazi yetu. Wanafunzi vile vile wamefanya kazi yetu kuwa rahisi sana kwa kuenzi na kupenda somo la Kiswahili.
Somo hili litawasaidia wanafunzi kuweza kuwasiliana vizuri bila shida yeyote na watu wengine hasaa wenzetu kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Tupende lugha ya kiswahili kwa sababu ni lugha iliyozaliwa hapa kwetu Afrika mashariki. Asante sana wote na karibuni sana.
Imeandikwa na mwalimu;
Anziya Benjamin na Mwalimu; Mukhone k.Christabel.